Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amefariki dunia hii leo Jumatatu ya Pasaka, Aprili 21, 2025,akiwa na umri wa miaka 88.
Taarufa za kifo cha Papa zimetangazwa na Mwadhama, Kardinali Farrell akisema amefariki akiwa katika makazi yake huko Casa Santa Marta, Vatican.

Amesema, Papa enzi za uhai wake alifundisha kuishi maadili ya Injili kwa uaminifu, ujasiri na upendo wa ulimwengu wote, hasa kwa ajili ya maskini zaidi na waliotengwa zaidi.”
“Shukrani nyingi sana kwa ajili ya kielelezo chake kama mfuasi wa kweli wa Bwana Yesu, tunaipongeza roho ya Papa Francisko kwa upendo wa huruma usio na kikomo wa Mungu Mmoja na wa Utatu,” alisema Farell.

Kifo cha Papa kimekuja chini ya saa 24 baada ya kujitokeza kwenye Uwanja wa St Peter’s Square mjini Vatican kwa ajili ya Jumapili ya Pasaka.
Alitoka akiwa kwenye kiti cha magurudumu na kupunga mkono kutoka kwenye baraza ya Basilica ya St Peter’s kwa umati wa watu waliokuwa wakishangilia na kusema: “Ndugu wapendwa, Pasaka njema.”

Hotuba yake ya Pasaka na baraka ilisomwa na Msaidizi wake alipokuwa ameketi, akitazama.
Baada ya baraka, alizungushwa kwenye uwanja, kupita katikati ya umati na msafara wake ulisimama mara kadhaa huku watoto wachanga wakiletwa ili awabariki.

“Ndugu wapendwa, kwa huzuni kubwa sina budi kutangaza kifo cha Baba Mtakatifu Francisko’,’ lilikuwa ni tangazo lililoshitua wengi na Jina la MUNGU lihimidiwe.