ASKOFU LIBENA: WATANZANIA TULINDE AMANI YA TAIFA LETU

Askofu wa Jimbo Katoliki Ifakara, Mhashamu Sulutaris Libena amewataka Watanzania kulinda na kudumisha amani na kuzingatia makubaliano na maelewano, kwa kuwa ndiyo msingi wa amani wa Taifa lao.

Askofu Libena ameyasema hayo leo Aprili 20, 2025, alipokuwa akitoa mahubiri wakati wa ibada ya Pasaka kitaifa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Andrea Mtume, Jimbo Katoliki lililopo Ifakara, mkoani Morogoro.

“Sisi kama nchi tunafurahia amani, tunasema tuna amani na ni kweli tuna amani. Hatuna vita hatuna magomvi, amani iendane na upendo, iwe zao la ukweli na amani inatokana na upendo. Amani inahitaji sana makubaliano na maelewano,” amesema Askofu Libena.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *