Chama cha Mapinduzi (CCM), kimeutaarifu Umma kuhusu mchakato wa ndani ya Chama wa uteuzi wa wagombea katika nafazi mbalimbali kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2025.
Taarifa iliyotolewa hii leo Aprili 10, 2025 iliyotolewa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla imeeleza kuwa zoezi hilo linatarajia kuanza Mei 1, 2025 na kumalizika Mei 15, 2025.
