Mahakama Kuu Mbeya leo jumatatu, Agosti 7, inatoa uamuzi wa kesi ya kupinga mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii,kati ya Serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai (IGA), unaohusu uwekezaji katika Bandari za baharini na katika maziwa nchini Tanzania.
Uamuzi huo umepangwa kutolewa leo Asubuhi hii na jopo la Majaji watatu walioisikiliza kesi hiyo linaloongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akishirikiana na Majaji Mustafa Ismail na Abdi Kagomba.
Kuelekea uamuzi huo leo hali ya ulinzi Mahakamani hapa imeimarishwa tofauti na siku zote wakati kesi hiyo ilipokuwa inasikilizwa. Askari Polisi wenye sare na wasio na sare na wengine wakiwa na silaha wanaonekana katika kona mbalimbali za mahakama hii kuimarisha ulinzi.