MNYIKA AMJIBU MCHOME, UNA NIA GANI?

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika amemjibu Kada wa Chama hicho Lembrus Mchome ambaye hivi karibuni aliibua hoja za uhalali wa uteuzi wa baadhi ya Viongozi.

Kupitia chapisho la mtandao wa X, Mnyika amesema, Februari 24, 2025 alimtumia ujumbe kuwa majibu ya barua yake yapo tayari na Mchome alisoma na akajibu.

“Badala ya tarehe 25 Februari 2025 kutaka Katibu Mkuu amjibu ni kwanini hakusema ukweli kuwa majibu yake yako tayari isipokuwa yeye mwenyewe hujayafuata au kupendekeza atumiwe kwa njia ipi mbadala,” aliandika Mnyika.

“Ana nia gani kuendelea kusema uongo dhidi ya Katibu Mkuu na dhidi ya Chadema? alichapisha akihoji Katibu Mkuu huyo.

Hivi Karibuni, Mchome alimuomba Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika kujibu barua yake ya malalamiko ya kupinga uteuzi wa viongozi wanane wa CHADEMA walioteuliwa na Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu Januari 22, 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *