Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema ameshangazwa na umaskini uliopo nchini kwake na kuwataka Wananchi kuimarisha vita dhidi ya tatizo hilo ikiwa wanataka kuishi maisha bora.
“Watu wengi sana katika nchi hii wameniambia kuwa wao hawajawahi kugusa milioni. Unaweza kufikiria katika miaka 64, bado kuna watu ambao hawajawahi kugusa ashilingi milioni?,” alishangaa Rais Museven.
Kauli hiyo ya Museven aliyoitoa hivi karibuni, imeibua mijadala katika mitandao ya kijamii, watu wakijaribu kukosoa namna watawala wa Kiafrika wanavyo wadhihaki raia wanao waongoza, kutokana na kauli zao.
