Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema wamefanikiwa kutoa Pikipiki ambazo ni nyingi kuliko watu waliowakuta katika ajali iliyotokea eneo la Kimara Stop Over, jijini Dar es Salaam.
Katika ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo Februari 14, 2025 Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia, baada ya Lori lenye namba za usajili T 908 BYM, kuacha njia na kuparamia Waendesha bodaboda.

Chalamila amesema, “taarifa ya Jeshi la Polisi itaweka bayana kuhusu idadi ya Pikipiki na ajali imetokea saa ngapi, chanzo cha ajali na taarifa nyingine za msingi.”
Awali, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mtatiro Kitinkwi alithibitisha kuwa bodaboda sita zilitolewa chini ya Lori na kwamba vyombo vya uokoaji vilikuwa vikiendelea kupambana ili kulinyanyua Lori lililoanguka.
