RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali na kumpangia kituo cha kazi Balozi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, imeeleza kuwa Dkt. Amina Suleiman Msengwa ameteuliwa kuwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali.

Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Msengwa alikuwa Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Dkt. Albina Chuwa ambaye amemaliza muda wake.

Jaji Dkt. Ntemi Nimilwa Kilekamajenga ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la
Masoko na Mitaji, akichukua nafasi ya Jaji Dkt. Deo John Nangela ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Prof. Aurelia Kamuzora ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Bodi ya Kahawa kwa kipindi cha pili na
Abdulmajid Nsekela ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
wa Bodi ya Chai Tanzania.

Nsekela anachukua nafasi ya Mustafa Hamis Umande ambaye amemaliza muda wake huku Prof. Hozen Kahesi Mayaya akiteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), akiteuliwa kwa kipindi cha pili.

Balozi Dkt. Habib Galuss Kambanga amepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *