AHUKUMIWA MIAKA 92 JELA KWA KOSA LA KUKUTWA NA MAJANI YA BANGI..

Taarifa kutoka Mkoani Mtwara imesema kuwa mnamo tarehe 29.01.2025 kwenye Mahakama ya Wilaya ya Nanyumbu ilimhukumu kifungo cha miaka 92 jela Salumu Yohana Mkonya (54) mkulima, mkazi wa Kijiji cha mnazi mmoja.

Makosa aliyohukumiwa nayo ni pamoja na, kupatikana na mbegu na majani ya mimea ya dawa za kulevya aina ya bangi, misokoto ya dawa za kulevya aina ya bangi pamoja na kupatikana na pombe haramu ya moshi. Mtuhumiwa huyo alikuwa akihifadhi dawa za kulevya pamoja na pombe haramu ya moshi katika nyumba yake kwa lengo la kujipatia kipato.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *