POLISI WABAINI CHANZO CHA AJALI YA BASI LA DODOMA JIJI FC

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Andrew Ngassa amesema chanzo cha ajali ya basi la Dodoma Jiji FC kutumbukia katika Mto Matandu kilitokana na Dereva wake, Erasto Nyoni kuwa kwenye mwendo kasi na kutochukua tahadhari ya ubovu wa barabara iliyoharibiwa na mvua msimu uliopita.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa hii leo Februari 12, 2025 imeeleeza kuwa wamebaini hayo baada ya Kwenda kukagua eneo la tukio na kusema basi hilo lililokuwa linatokea Ruangwa lilibeba watu 36, wakiwemo wachezaji 24 na watu benchi la ufundi 12.

Amesema, “Gari lilikuwa linarudi Dodoma kupitia Dar es Salaam lilikuwa limebeba watu 36 miongoni mwao wachezaji walikuwa 24 pamoja na benchi la ufundi watu 12. Lilipofika kwenye daraja la Matandu lilimshinda dereva na kutumbukia katika mto huo, na kusababisha majeruhi wanane.”

Februari 10, 2025 majira ya saa tatu asubuhi katika Kijiji cha Matandu Wilayani Kilwa, basi hilo lilipata ajali wakati timu hiyo ilipokuwa ikisafiri kutoka Wilayani Ruangwa kwenye mchezo wake na timu ya Namungo FC ambao walitoka sare pacha ya 2-2.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *