Kupitia ukurasa wake wa Insta, afisa Habari wa Yanga SC, Ally Shaban Kamweamechapisha andiko linalowachambua Wachambuzi wa soka hapa Bongo.
Kamwe anasema, “leo Baunsa wa Kolo Kakosa Goli Yeye na Nyavu, Lakini husikii sauti ya Mchambuzi yoyote akimponda, Kuko kimya kabisa.
“Kwetu Prince Dube kwenye mechi ambayo anafunga Goli 2 na Kutoa asisti, Timu inashinda Goli 6, Wachambuzi wanachukua goli moja alilokosa DUBE na kuweka Mjadala.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/f87b512e-23bb-4d55-a1fe-3f9fc1291e9b.jpg)
Na kwa bahati mbaya mno, Wanayanga Tunaingia kwenye mtego wa kumponda mchezaji wetu bila kujua kama tunazidi kumpotezea kujiamini.
Sikatai, Tuna shauku afunge zaidi na zaidi Lakini Duniani hakuna mshambuliaji anayefunga Kila nafasi.
Inatokea kwenye Football, Straika kukosa nafasi. Lakini kwa Hapa Bongo, Dube amekuwa Mhanga mkubwa wa hilo
Kama mtu ni mgeni wa Ligi, akisoma kinachoandikwa kuhusu Dube anaweza kudhani hana goli hata moja. Kumbe ndio Straika mwenye Takwimu nzuri zaidi kwenye Ligi mpaka sasa.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/5b9dfb20-7420-4321-a570-1f8ba74859a9.jpg)
Goli 7, Asisti 4… Lakini anavyoandikwa na Kuchambuliwa kama hamna alichofanya.
Niwaombe Wananchi wenzangu, Tuko katikati ya uwanja wa Mapambano. Vita yetu ya Ubingwa Msimu huu ni KUBWA SANA
Mafanikio Yetu misimu hii Mitatu imetujengea Maadui wengi kweli kweli. Tunatakiwa kuwa MAKINI na KILA AJENDA tunayoletewa Mezani na Baadhi ya Wachambuzi
Huu ni wakati tunaotakiwa kuwa Kitu kimoja, kushikamana na Kusapoti wachezaji wetu.. Furaha Tunayotaka kuipata Msimu huu, Wao ndio WATATULETEA.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/464204170_1079039770476804_2360281927623553916_n.jpg)
NAWAOMBA SANA, TUSIMAME NA PLAYERS WETU, TUWALINDE NA TUWASHANGILIE ILI WAWE NA NGUVU YA KUTUPAMBANIA ZAIDI NA ZAIDI
Imagine Goli alilokosa Baunsa Leo ndio angekosa Dube, Makala zingeandikwa Usiku kucha ili Kumtia Presha na kumpunguzia Umakini Dube
DUBE NI SILAHA YETU MUHIMU SANA MACHI 8
Makolo wanajua Hilo ndio Maana kuna Nguvu Kubwa mno inatumika kumpunguzia Kujiamini.
Tushtuke Wananchi,” alimaliza Kamwe.