Zaidi ya mabomu 170 yanayosadikika kuwa yalisalia mara baada ya Vita vya Pili vya Dunia, yamepatikana chini ya ardhi katika uwanja wa michezo wa Watoto kaskazini mwa Nchi ya Uingereza, huku kukiwa na wasiwasi kwamba zaidi huenda yapo katika maeneo mengine zaidi.
Mabomu hayo, yaligunduliwa wakati mradi wa ujenzi ulipokuwa ukiendelea wa kukarabati Uwanja wa michezo wa Scotts Park huko Wooler, mji mdogo wa Northumberland, ambao uko karibu na mpaka na Uskoti.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/b9ff21a3-7caa-4a65-9a7b-9b9b8d3a3b16.jpg)
Taarifa ya vyombo vya Habari imeeleza kuwa, “Wafanyakazi wamepata kitu cha kutiliwa shaka Januari 14, walipokuwa wakichimba msingi. Ilibadilika kuwa bomu la mazoezi, au bomu lisilolipuka ambalo hutumiwa kwa mafunzo lakini bado linaweza kuwa na madhara.”
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/bombs-in-storage-1024x576.webp)
Maafisa wa Baraza la Parokia ya Wooler, waliisajili Kampuni ya Brimstone Site Investigations, ambayo ni mtaalamu wa silaha zisizolipuka, kuchunguza eneo hilo.
Brimstone iliwasili Januari 23 kwa kile ambacho kilipaswa kuwa uchunguzi wa siku mbili, lakini hivi karibuni ikawa dhahiri kwamba tatizo lilikuwa kubwa zaidi kuliko ilivyotarajiwa.