Bangladesh inakabiliwa na wimbi jipya la ghasia wakati wanachama wa vuguvugu la maandamano ya wanafunzi lililopindua serikali ya kimabavu ya Sheikh Hasina mwezi Agosti walipambana tena na wafuasi wake, wakionyesha udhaifu wa nchi inayojitahidi kujijenga upya.
Vurugu hizo, zilianza wiki iliyopita, baada ya Chama cha kisiasa cha Bi Hasina, Waziri Mkuu wa zamani, kusema kwamba angehutubia Wanafunzi na raia wa Bangladesh kupitia sauti kutokea India, ambapo amekuwa akiishi tangu kuondolewa kwake Agosti 5, 2024.
Waandamanaji walisema hotuba hiyo ya mtandaoni itachochea vurugu huku maelfu ya Wanafunzi wakichoma moto jumba la makumbusho ambalo zamani lilikuwa makazi ya baba yake Bi Hasina, Sheikh Mujibur Rahman, ambaye ni mwanzilishi wa Bangladesh.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/Screenshot_20250210-210644_Chrome.jpg)
Mapigano kati ya waandamanaji Wanafunzi na wafuasi wa Ligi ya Awami yalidumu siku tatu kabla ya Serikali ya mpito inayoongozwa na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Muhammad Yunus kuanzisha “Operesheni Devil Hunt,” na kuleta Polisi wa Bangladesh na vikosi vya kijeshi ili kukabiliana na wale wanaounga mkono, huku ligi ya Awami ikitishia kuandamana dhidi ya vitendo vya Wanafunzi.
Baada ya hotuba ya moja kwa moja ya Bi. Hasina ambayo aliwakumbusha Wabangladeshi kuhusu kujitolea kwa babake na jinsi nchi hiyo ilivyostawi wakati wa utawala wake, waandamanaji na wafuasi wa Ligi ya Awami katika eneo la Dhaka walianza kushambuliana.