Frank Aman – Geita.
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Teddy Thomas (25), mkazi wa Katoro Wilayani Geita, Mkoani Geita amefikishwa katika kituo cha afya cha kata ya Katoro baada ya kudaiwa kupigwa na mume wake na kumsababishia maumivu makali ya mwili akimtuhumu kumkuta na namba ya Mwanaume mwingine tukio ambalo limefanyika Februari 7, mwaka huu 2025
Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Katoro, Dkt. Yohana Kitutu amethibitsha kumpokea mwanamke huyo na kumpatia huduma ya kwanza na kwamba hali yake inaendelea vizuri huku akieleza kutoa rufaa ya kwenda hopstali ya rufaa Geita.
Nkimbili Mabula ambaye ni Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) tawi la Lutozo, Katoro amelaani tuki hilo huku akiomba mamlaka zichukue hatua kali ili kukomesha vitendo vya namna hiyo
Hata hivyo, Jambo fm ilifika Polisi Mkoa wa Geita ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita SACP. Safia Jongo hakuweza kupatikana na simu yake iliita bila mafanikio.