DODOMA JIJI FC WAPATA AJALI SOMANGA

Taarifa kutoka Mkoani Lindi zinaeleza kuwa Basi la Timu ya Dodoma Jiji FC, limepata ajali katika eneo la Nangurukuru kuelekea Somanga, likiwa likitokea mjini Ruangwa ambako jana Februari 9, 2025 ilicheza dhidi ya Namungo FC na kupata sare pacha ya 2-2.

Mashuhuda wa ajali hiyo wakisimulia tukio wamesema Basi hilo limetumbukia kwenye Mto, ingawa hakuna madhara kwa Wachezaji zaidi ya majeraha kwa baadhi yao na kwamba wamedai kuna uharibifu wa mali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *