KUUNGUA OFISI YA TRA KARIAKOO HAKUNA MADHARA.

Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda akizungumza na Vyombo vya habari, amesema Wafanyakazi wote waliokuwa kwenye jengo lililowaka moto leo, Kariakoo jijini DSM wametoka salama na hakuna madhara kwa taarifa za walipa kodi sababu sehemu iliyoungua ni sehemu ya matumizi ya kawaida.

Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji na Msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi, amesema kuwa askari wa Jeshi hilo wamefanikiwa kuuzima moto katika jengo la ofisi za TRA Kariakoo.

Nzalayaimisi ameongeza kuwa hakuna madhara yoyote kwa binadamu yaliyotokana na ajali hiyo ya moto na kwamba chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *