MAJI YA MVUA YAUWA WAWILI MORO, POLISI YATOA TAHADHARI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limethibitisha vifo vya watu wawili vilivyotokea katika maeneo tofauti kwa sababu za Mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani humo, huku likitoa tahadhari kwa Wananchi kuacha kujaribu kina cha Maji.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro iliyotolewa hii leo Januari 30, 2025 imeeleza kuwa tukio la kwanza limetokea usiku wa kuamkia Januari 30, 2025 katika mtaa waMajengo mapya, kata ya Lukobe, Manispaa ya Morogoro, ambapo mtu mmoja Hashim khasimu Juma (43), mkazi wa Kihonda B alikufa maji alipokuwa anajaribu kuvuka mto ambao ulikuwa umejaa maji.

Katika tukio la pili, Taarifa hiyo imeeleza kuwa limetokea Januari 29, 2025 mchana katika mtaa wa Mafisa, uliopo Kata ya Mafiga, Manispaa ya Morogoro, ambapo ulipatikana mwili wa mwanaume, anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 35-40 ukiwa ndani ya maji yaliyotuama akiwa tayari amefariki.

“Mtu huyo hajaweza kufahamika na inadhaniwa kuwa alishindwa kujiokoa baada ya kudumbukia ndani ya shimo hilo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa kiasikikubwa. Mwili huo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti ili kutoanafasi kwa ndugu kuutambua,” ilieleza taarifa hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *