Punguzeni semina, wananchi wapate huduma vituoni

Waziri Wa Afya, Ummy Mwalimu Amewataka Wataalamu Wa Afya Nchini Kupunguza Semina Ili Kuwa Na Muda Zaidi Wa Kutoa Huduma Bora Za Matibabu Kwa Wananchi.

Waziri Ummy Ameyasema Hayo Leo Julai 10, 2023 Katika Ziara Yake Mkoani Simiyu Wakati Akizungumza Na Viongozi Wa Mkoa Huo Chini Ya Mkuu Wa Mkoa Dkt. Yahaya Nawanda.

“Wataalamu Wa Afya Punguzeni Semina Maana Mmekuwa Na Semina Nyingi Hadi Kupelekea Wagonjwa Kukosa Huduma Kwa Wakati Na Kumekuwa Na Msomgamano Mkubwa Katika Vituo Vya Kutolea Huduma Za Afya Sababu Ya Semina”, Amesema.

Aidha, Amesema Kuwa Katika Utolewaji Wa Huduma Za Afya Nchini Hakuna Kilichosimama Kwakuwa Serikali Imejenga Majengo Ya Hospitali, Imetoa Dawa Na Vifaa Tiba, Hivyo Ni Jukumu La Wataalamu Wa Afya Kutoa Huduma Bora Patika Vituo Hivyo.

Pia, Waziri Ummy Mwalimu Ameutaka Uongozi Wa Mkoa Wa Simiyu Kuwasimamia Madaktari Ili Wafanye Kazi Kwa Weledi Kwa Kuangalia Historia Ya Mgonjwa Ili Apate Huduma Sahihi Na Kwa Wakati.

Ameongeza Kuwa, Lengo La Serikali Ni Kutoa Huduma Bora Za Afya Kwa Watanzania Na Kwa Mara Ya Kwanza Serikali Imetoa Hela Za Dawa Kwa Asilimia 100, Hivyo Amevitaka Vituo Vyote Vya Afya Kuwa Na Dawa Zote Muhimu Ili Kumsaidia Mwananchi Kupata Huduma Za Matibabu Kwa Wakati.

Hata Hivyo, Waziri Ummy Ametoa Rai Kwa Watoa Huduma Nchini Kuzingatia Utumiaji Wa Lugha Nzuri, Weledi Na Maadili Na Kuzingatia Viapo Vya Wataalam Wa Afya Wakati Wa Kuwahudumia Wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *