Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, ameongoza juhudi mpya za kikanda kwa kuhimiza mshikamano wa nchi za Afrika katika kuhakikisha upatikanaji wa nishati endelevu na nafuu kwa kila mwananchi ifikapo mwaka 2030.

Akizungumza hii leo Januari 27, 2025, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nishati wa Nchi za Afrika jijini Dar es Salaam, Dkt. Biteko amemkutano huo ni fursa muhimu kwa bara la Afrika kuimarisha mikakati ya kuongeza upatikanaji wa umeme na matumizi ya nishati safi.

“Tuna jukumu la pamoja kuhakikisha tunafanikisha lengo la kuwafikishia umeme wa uhakika watu milioni 300 katika ukanda wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ifikapo mwaka 2030,” alisema Dkt. Biteko.

Kufanyika kwa Mkutano huo ni juhudi za pamoja zinazoongozwa na Wakuu wa Nchi za Afrika, kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Benki ya Dunia, na wadau wa maendeleo, ili kukabiliana na changamoto ya nishati inayowakabili Waafrika milioni 600 ambao bado hawajafikiwa na umeme.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *