Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambaye pia ni Muandaajia wa Matamasha ya muziki wa injili, Alex Msama ametoa maoni yake kuhusiana na kitendo cha Msanii wa nyimbo za Injili Nchini Goodluck Gozbert kuchoma moto gari analodaiwa kupewa zawadi na Nabii Mkuu Geor Davie wa Arusha huku akiimkata kuomba radhi.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa kitendo cha Muimbaji wa nyimbo za injili ambaye ni kijana wangu mimi, nathubutu kutamka hivyo sababu namjua Goodluck Gozbert, kitendo chake cha kuchoma gari moto alilopewa na mtumishi wa Mungu Nabii Mkuu Geor Davie, mimi nimesikitishwa sana na kitendo kile sababu sio kitendo kizuri na naweza kusema kuwa halijui neno,” alisema Alex Msama
“Alichofanya ni kitendo ambacho sio kizuri kwa sababu anaposema nachoma gari moto sababu anaona mavitu ya ajabu kwenye gari ni kitu ambacho naweza kusema hajasimama kwenye neno, mtu wa Mungu ambaye amesimama kwenye neno na mtumishi wa Mungu ambaye Mungu yupo ndani yake hawezi kuyumbishwa na jambo lolote,
iwe nyumbani kwake, iwe kwenye biashara yake iwe kwenye gari yake, kama gari lile lina shida angeliombea kama ameshiba kiimani kila kitu kingeweza kutoka na angelitumia kama kawaida ” Alex Msama
Itakumbukwa Desemba 2021 Nabii Mkuu Geor Davie alimzawadia Goodluck Gozbert zawadi ya gari aina Marcedes Benz sambamba na pesa taslimu Tsh milioni 2 kutokana na kuvutiwa na kufurahishwa na kazi zake.