Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limeutaarifu umma juu kufungwa kwa baadji ya barabara, ili kupisha misafara ya Viongozi kutokana na Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Nishati, ambao Wakuu wa Nchi na Mawaziri wa Fedha na Nishati wa Afrika watashiriki kuanzia tarehe Januari 27-28, 2025.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro imesema Barabara ambazo zitafungwa ni ile ya Nyerere kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda katikati ya Jiji na Barabara ya Sokoine, Kivukoni na Lithuli kuanzia taa za Gerezani
kwenda Hoteli ya Johari Rotana, Hyatt Regency hadi Ikulu.
Nyingine ni Barabara ya Ohio kutokea Kivukoni kwenda Hoteli ya Serena, Barabara ya Ghana kutokea barabara ya Ohio kwenda Hoteli ya Onomo, Barabara ya Bibi Titi kutokea makutano ya barabara za Ohio na Ally Hassan Mwinyi kwenda Hoteli ya Crowne.
Aidha, taarifa hiyo imefafanua kuwa pia Barabara ya Azikiwe kwenda Hoteli ya Four Points, Hoteli ya Golden Tulip City Center na Hoteli ya Holiday Inn nazo zitafungwa.
Nyingine ni Barabara ya Morogoro kutokea Sokoine kwenda Hoteli ya Tiffany No.1 , Barabara ya Makunganya kutokea Azikiwe kwenda Hoteli ya Tiffany No. 2.l, Barabara ya Garden kutokea barabara ya Lithuli kwenda Hoteli ya Southern Sun pamoja na Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa JNICC.
Katika kipindi chote cha Mkutano, watumiaji wengine wa barabara
wanashauriwa kutumia barabara za Uhuru, Kawawa kupitia Magomeni, Kigogo
kuelekea Temeke, barabara ya Morogoro na Msimbazi, Morogoro na Lumumba na kwa wale wanaotokea maeneo ya Chanika wanashauriwa kutumia njia mbadala ya mradi wa SGR, ili warokee barabara ya Mandela na Uhuru.
Taarifa zaidi ya Jeshi la Polisi na kujua njia mbadala, ni kama inavyoonekana katika viambata.