Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amevikumbusha Vyuo Vikuu Viliyopo nchini Umuhimu wa kujikita katika Kufanya Tafiti ambazo zitatoa Ufumbuzi wa Changamoto za Kijamii na kuzisambaza kwa Watumiaji.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo katika Mahafali ya 24 ya Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al Sumait Chukwani Wilaya ya Magahribi B, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Ametoa wito kwa Viongozi wa Vyuo Vikuu kuendelea Kujenga Uwezo wa kufanya Tafiti kwa Wafanyakazi kwa kutumia Fursa ziliyopo pamoja na Kushirikiana na Vyuo Vikuu vya vyengine vyenye Wataalamu Waliobobea katika Tafiti kwa ajili ya kuwajengea Uwezo Wataalamu Wazalendo.
Rais Mwinyi pia amesema muhimu kwa Wizara na Idara za Serikali kushirikiana na Vyuo Vikuu kufanya Tafiti na kutumia Tafiti mbalimbali kuleta Maendeleo katika Nyanja za kijamii,Kiuchumi na Kiutamaduni.
Rais Dkt. Mwinyi amesema Serikali inathamini juhudi za Chuo Kikuu cha Abdulrahnan Al Sumait katika Utoaji wa Elimu kwani kunachangia Nguvu kazi na Ongezeko la Waatalamu Wazalendo katika Sekta Mbalimbali za Umma na Kijamii.
Ameahidi Serikali Kuendelea kutoa Ushirikiano wa kiwango cha juu ili Chuo hicho Kifikie malengo ya Kuanzishwa kwake.
Wahitimu 304 katika fani mbalimbali wamehitimu Katika Mwaka wa Masomo 2023-2024 ,Wanawake wakiwa 203 na 101 Wanaume, na kufikisha Wahitimu 4,993 waliohitimu katika Chuo hicho tangu Kuanzishwa kwake Mwaka 1998.