Wafanyabiashara,Wawekezaji na Wabunifu hapa nchini wametakiwa kujiunga katika mfumo wa kidigitali wa Haippa Marketing Solution mfumo ambao utawasaidia katika kufanya uwekezaji katika shughuli mbalimbali wanazozifanya.
Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Haippa hapa nchini Samira Ally wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo mkoani Mwanza ambapo amesema kupitia mfumo huo mfanyabiashara na mbunifu anaweza kuitambulisha biashara yake kwa wateja wapya huku pia akiwa na uwezo wa kupata mkopo kutoka katika kampuni hiyo ili aweze kukuza na kuendeleza biashara yake.
Aidha Samira pia ameongeza kwa kusema kua kampuni hiyo imelenga kuchochea ubunifu kwa wafanyabiashara ili waweze kukuza biashara zao na kuwafikia watu waliopo ndani na nje ya Africa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni hiyo Boniphase Ndengo amesema kampuni hiyo imelenga kuwainua wafanyabiashara hapa nchini hii ni kupitia mikopo ya dhadura mikopo ambayo itasaidia kutanua wigo wa biashara wanazozifanya.
Pia Mkurugenzi huyo ameongeza kwa kusema kua kampuni hiyo imelenga kuwajengea uwezo vijana wanaomaliza elimu za vyuo ili wawe na uwezo wa kusimamia sekta binafsi hali ambayo itasaidia kupunguza tatizo la ajira hapa nchini.
Nae Mwenyekiti wa chemba ya Wafanyabiashara mkoa wa Mwanza Gabriel Kenene amesema anaipongeza kampuni hiyo kwa ubunifu mkubwa iliyoifanya kwani uwepo wa mfumo huo wa kidigitali unakwenda kuwainua Watanzania ambao walikosa fursa ya kuendeleza biashara zao.