Tume ya Uwiano na Utangamano nchini Kenya (NCIC), imependekeza kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa zaidi ya wabunge 10 ambao wanadaiwa kutia matamshi yenye chuki na yanayoendelea kuigawanya nchi hiyo.
NCIC imesema imehitimisha uchunguzi na kumkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya upelelezi wa Jinai, kwa ajili ya Wabunge hao ambao ni Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi, Mbunge wa Daadab Farah Maalim na Mbunge wa Webuye Magharibi Dan Wanyama.
Mwenyekiti wa tume hiyo Samuel Kobia amesema matamshi ya Wabunge hao yamesabahisha Kaunti za Nairobi, Nakuru, Mombasa, Kisumu na Kiambu kuwa na ongezeko la makundi yanafanya uhalifu.
Hata hivyo wadadisi wa mambo wanasema licha ya mapendekezo hayo na mengine ambayo yaliwahi kutolewa, Viongozi na wanasiasa hasa wanaounga mkono serikali iliopo madarakani huwa hawawajibishwi.