Serikali Kupitia Tume Ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Imeongeza Bajeti Ya Mapambano Dhidi Ya Ukimwi Kutoka Shilingi Bilioni 14 Katika Mwaka Wa Fedha Ulioisha Hadi Bilioni 25 Katika Mwaka Mpya Wa Fedha 2023/2024 Ili Watu Wanaoishi Na Virusi Vya Ukimwi Waweze Kupata Dawa Kwa Uhakika Na Kuendeleza Shughuli Zao.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Naibu Waziri Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge Na Uratibu Ummy Nderiananga, Alipowatembelea Watu Wanaoishi Na Virusi Vya Ukimwi Katika Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Ambapo Alisema Lengo La Serikali Ni Kuona Waviu Wanaendelea Vyema Na Maisha Yao Huku Wito Ukitolewa Kwa Wanaume Kujiunga Kwenye Vikundi Pindi Wanapobainika Kuwa Na Maambukizi.