Mbappe apokelewa kifalme nchini Cameroon

Nyota wa PSG na mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Kyllian Mbappe amepokelewa kifalme wakati akifanya ziara yake ya siku tatu huko nchini Cameroon.

Katika ziara yake hiyo, Mbappe ameambatana na baba yake mzazi Bw. Wilfred Mbappe ambaye ni mzaliwa wan chi hiyo ya Cameroon.

Aidha, akiwa nchini humo Mbappe anatarajiwa kucheza mchezo mmoja wa kirafiki na timu moja ya nchini humo kabla ya kuhitimisha ziara yake hapo kesho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *