MAUAJI YA KUSHANGAZA: SANGOMA AMSALITI MTEJA WAKE KWA POLISI, MAITI ZAFUKULIWA

Ama kweli sasa nasadiki ya Wahenga ambao walipata kusema “Dunia tambara bovu” yaani Ulimwengu huu unageukia kitu kingine kabisa!

Mwaka 2016 – kuna dada anaitwa Pamela Ncumisa Selani, raia wa Afrika Kusini aligundua kuwa mpenzi wake kutoka Malawi Michael Changisa alimpa maambukizi ya VVU️.

Alikasirika lakini kumbe Ncumisa alikuwa na mpenzi mwingine ‘super sub’ kutoka Zimbabwe, anaitwa Michael Phiri, akampigia simu akimwomba amsaidie “kummaliza” Changisa.

Pamela Ncumisa Selani wakati akiwa katika Mahakama ya Gauteng, Pretoria Nchini Afrika Kusini.

Phiri kwa hofu ya kupoteza penzi alikubali na akafanya kazi hiyo, kisha walimzika Changisa kwenye uwani mwa nyumba ya Ncumisa wakashinda vita.

Baadaye mwaka 2017- Phiri akahamia kabiss na kukaa na Ncumisa aliyekuwa na Watoto wawili (miaka 17 & 10), katika nyumba yake.

Sasa Phiri akaanza kumnyanyasa Ncumisa, hivyo Ncumisa na mtoto wake (17) wakaona isiwe tabu, wakala njama na wakamuua na kumzika Phiri juu ya mwili wa Changisa kule uwani kwenye kaburi la mpenzi wa kwanza, kisha wakapongezana.

Siku zikasogea ikafika mwaka 2018 – Mtoto wa Ncumisa sasa akatikima miaka 18, mbaya zaidi akawa mtumiaji mkubwa wa dawa za kulevya.

Na mara kwa mara akamfuata mama yake akimuomba pesa za dawa za kulevya huku akitishia kuwaambia Polisi walichomfanyia Phiri.

Ncumisa akaona ‘dogo anazingua’ akajishauri akaona ili aishai kwa amani ni lazima aumuue mwanaye na alipofanikiwa akamzika juu ya mwili wa Phiri, ukiwa ni mwili wa tatu katika kaburi moja.

Miaka miwili baadaye yaani 2020 Mtoto aliyebaki wa Ncumisa, akaanza kuugua na haikufahamika mara moja ana maradhi gani na mama yake akahangaika sana bila mafanikio.

Walishauriana na wakaamua kumtembelea mganga wa kienyeji, ili kujua anaumwa nini, mganga kabla ya kupiga manyanga walihojiana sana bula mafanikio.

Wakati wa mashauriano, mama alichepuka nje kidogo hivyo mwana akaona mwanya ndiyo huo, akamwambia mganga kuhusu mauaji yake yaliyotokea katika nyumba ambayo aliamini kuwa yanahusiana na “ugonjwa” wake.

Shimo lililofukiwa miili ya watu watatu baada ya kutekelezwa kwa mauaji hayo, ikizikwa kwa nyakati tofauti.

Mganga wa kienyeji badala ya kuita ‘mizimu’ akaona isiwe tabu mbio kituo cha Polisi kumripoti Ncumisa.

Dada huyu Pamela Ncumisa Selani alikamatwa siku hiyohiyo, hatimaye baada ya upelelezi na kupatikana kwa ushahidi alihukumiwa vifungo vitatu vya maisha.

Ilikuwa ni Julai 29, 2024 ambapo Mahakama kuu ya Gauteng huko Pretoria ilichukua uamuzi huo kwasababu Ncumisa alipatikana na hatia ya kuwaua wapenzi wake wawili na mtoto wake mmoja wa kiume.

Ama kweli, ndio maana wahenga waliyaongea mengi sana, mara kuwa uyaone, asiyesikia la mkuu, mtoto umleavyo, asiyefunzwa na mamaye nk. lakini hii yote ni kwamba hakuna siri ya wawili au zaidi, ladamu nzito.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *