MALARIA HUUWA WATU LAKI SITA KILA MWAKA – WHO

Karibu dozi milioni 10 za Malaria zilipelekwa barani Afrika katika mwaka wa kwanza wa utoaji wa kawaida wa chanjo kote barani humo huku WHO ikisema ugonjwa huo huuwa watu 600,000 kila mwaka.

Taarifa ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Chanjo – GAVI, umeyasema hayo na kudai kuwa zaidi ya dozi milioni 9.8 zimetolewa, na kusema angalau watoto milioni tano wamepata ulinzi wa kutosha.

Programu hiyo, inalenga kutoa chanjo nne kwa kila mtoto na kusisitiza kwamba kila mara ulilenga kuwafikia watu wanaokabiliwa na kitisho zaidi katika kila nchi.

Shirika la Afya ulimwenguni, WHO limesema ugonjwa wa Malaria huua karibu watu 600,000 kwa mwaka, wengi zaidi kutoka Afrika na waathirika wakubwa wakiwa ni watoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *