UMEME KUKATIKA KATIKATI YA UCHAGUZI WA CHADEMA – TANESCO YATOA SABABU

Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), limeutaarifu umma juu ya hali yaupatikanaji wa umeme katika Jiji la Dar es Salaam kwa kusema ni nzuri licha ya kuwa na maboresho mbalimbali ya miundombinu ya umeme inayoendelea kwenye baadhi ya maeneo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano na Huduma kwa Wateja Makao Makuu Dodoma, imeeleza kuwa hii leo, majira ya saa 6:56 mchana hadi 6:58 mchana kulitokea hitilafu ya dharura katika njia ya umeme ya Mlimani City, ambapo wataalamu wao walirekebisha na kurejesha huduma katika eneo hilo kwa haraka.

Aidha, TANESCO imewahakikishia wateja wake kuwa hali ya upatikanaji wa umeme ni nzuri na kwamba wanaendelea kushirikiana na wadau wote, ili kuwezesha shughuli za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *