Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti atakuwa kocha mkuu wa Brazil kuanzia Juni 2024.
Viongozi wa Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) wameelezea nia ya kusubiri msimu mmoja na kisha kumleta Ancelotti kuongoza timu hiyo katika Kombe la Dunia la mwaka 2026.
Hivi sasa Fernando Diniz atahudumu kama kocha mkuu wa timu hiyo ya taifa kwa mkataba wa miezi 12.