Rais Samia Suluhu Hassan Ameuhakikishia Umoja Wa Ulaya (EU) Kuwa Miradi Yote Iliyoifadhili Itafanyika Kwa Weledi Na Ufanisi Mkubwa Huku Akisema Kuwa Tanzania Itaendelea Kuwa Na Ushirikiano Wa Karibu Na Umoja Huo Kwa Ajli Ya Manufaa Ya Pande Zote Mbili.
Kauli Hiyo Ameitoa Jijini Dodoma Leo Jumanne Julai 04, 2023 Alipohudhuria Hafla Ya Kupokea Fedha Za Msaada Wa Bajeti Kuu Ya Serikali Kutoka Umoja Huo Ambapo Mikataba Mitatu Imetiwa Saini.
Aidha Rais Samia Amemshukuru Balozi Wa Umoja Huo Nchini Tanzania, Manfredo Fanti Ambaye Anakaribia Kumaliza Muda Wake Akisema Kufanya Naye Kazi Kumezaa Matunda Huku Akimtaka Kuendelea Kuwa Balozi Mwema Na Mzuri.