RAIS MTEULE WA MAREKANI DONALD TRUMP AHUKUMIWA…..

RAIS mteule wa Marekani, Donald Trump leo ameingia kwenye historia baada ya kusomewa hukumu ya kesi iliyokuwa ikimkabili na kumfanya kuwa Rais wa kwanza wa Marekani kuhukumiwa kwa makosa ya jinai.

Hukumu ya Trump ilitolewa jana Ijumaa Januari 10, 2025, lakini bahati nzuri Trump hatotumikia kifungo chochote wala kutakiwa kulipa faini katika shtaka la matumizi mabaya ya fedha kwa kumhonga mcheza picha za utupu ili asitoe taarifa za kushiriki ngono na mwanasiasa huyo.

Juan Merchan ambaye ni Jaji wa Mahakama Kuu nchini humo, amesoma hukumu ya kesi ya Trump huku hukumu hiyo ikiwa haijaambatana na adhabu yoyote dhidi ya Rais Mteule na bilionea huyo wa Marekani.

Hukumu hiyo imesomwa ikiwa ni siku moja tangu Mawakili wa Donald Trump wawasilishe ombi la kuitaka Mahakama hiyo ya juu nchini Marekani kutosoma hukumu hadi Rais huyo mteule atakapoapishwa, ombi ambalo lilikataliwa.

Donald Trump anatarajiwa kuapishwa siku ya Januari 20, 2025 na kuanza kulitumikia taifa hilo kwa mara ya pili akipokea kijiti kutoka kwa mtangulizi wake na Rais wa sasa wa taifa hilo Joe Biden.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *