Jeshi la Polisi Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limethibitisha kumshikilia aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chadema na balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt. Wilbrod Slaa.
Kamanda wa Polisi Kanda maalum Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema ”Daktari yupo, tuko naye na tumekuwa na mahojiano naye kwa baadhi ya mambo na yanakwenda vizuri kwa hiyo tunaiangalia mifumo ya kisheria inatuelekeza ni nini cha kufanya na taarifa kamili zitatolewa baadaye,” amesema Kamanda Muliro.
Taarifa ya kukamatwa kwa Dkt. Wilbroad Slaa ilisambaa kupitia mitandao ya kijamii, ikisikika sauti ya mwanasiasa huyo akizungumza kuhusu kukamatwa na Jeshi la Polisi na kwamba anapelekwa katika Kituo cha Polisi cha Mbweni, Dar es Salaam.