MZIZE ACHAGULIWA KUWA MCHEZAJI BORA WA WIKI WA CAF…

Clement Mzize Mshambuliaji wa Yanga, amechaguliwa na shirikisho la soka Afrika (CAF) kuwa mchezaji bora wa wiki baada ya kuwa sehemu ya Wachezaji waliofanikisha Yanga kupata ushindi wa Goli 3-1 dhidi ya TP Mazembe ya Congo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwenye mchezo huo, Yanga ilianza kufungwa goli 1 kisha kutoka nyuma na kupata ushindi ambapo Mzize alifunga Goli mbili kati ya Goli tatu zilizofungwa siku hiyo.

CAF imemtangaza Mzize baada ya kuwashinda nyota wengine waliokuwa wakichuana kwenye orodha ya wachezaji waliofanya vizuri wiki hii. 

Mabao mawili alioyafunga dhidi ya Mazembe yanamfanya Mzize kufikisha jumla ya Goli mbili kwenye mshindano haya msimu huu baada ya kucheza mechi tatu. 

Kwenye msimamo wa kundi, Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye kundi A ikiwa na pointi nne, nyuma ya MC Alger iliyo nafasi yapili kwa pointi tano na vinara Al Hilal wenye pointi 10, timu ya mwisho ni TP Mazembe ambayo ina pointi mbili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *