JESHI LA POLISI LAMSAKA KIJANA ALIEJIREKODI ANAUZA MTOTO…..

Jeshi la Polisi Tanzania, limetangaza kumtafuta kwa kuendesha msako nchi nzima mtu ambaye ametengeneza na kusambaza picha mjongeo (video clip) akitangaza kuwa anamuuza mtoto aliyembeba kwa shilingi milioni moja na laki sita.

Pamoja na hayo Jeshi la Polisi limesema msako huo utahakikisha anakamatwa ili hatua nyingine za kisheria ziweze kufuata Aidha, Jeshi la Polisi limelaani kitendo hicho cha kikatili na kilicho kinyume na sheria.

Mbali na hiyo Polisi imetoa wito kwa wananchi kuendelea kufichua vitendo kama hivyo, kuvilaani na kuvikemea kwani vinaweza kusababisha madhara kwa watoto ili hatua zichukuliwe kabla madhara hayajatokea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *