Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewafahamisha Wananchi kuwa kuwa Serikali inakuja na Mpango Mkubwa wa Usafiri utakaoifanya Zanzibar kuwa na Usafiri wa Kisasa wenye Huduma Bora.
Rais Mwinyi amesema kuwa mpango huo utajumuisha ujenzi wa Vituo vya Kisasa vya Mabasi katika Maeneo ya Chuini, Jumbi, Mwera na Mwanakwerekwe pamoja na Kijangwani, Malindi na Mnazi Mmoja kwa eneo la Mjini kasisitiza kuwa kabla Mwisho wa Mwaka huu 2025 Zanzibar itaanza kutumia Mabasi Ya Umeme.
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo wakati akifungua Kituo cha Mabasi Kijangwani Wilaya ya Mjini,Mkoa wa Mjini Magharibi kituo kilichojengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF).