Meneja wa habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa hawana mpango wa kuhama KMC Complex na kuwataka Wanasimba kupuuza maneno hayo ambayo yanatengenezwa.
Ahmed Ally ameyasema hayo baada ya kuwepo kwa taarifa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikidai klabu ya Simba imeandika barua kwenda Bodi ya Ligi Kuu [TPLB] ya mabadiliko ya uwanja wao wa nyumbani kutoka uwanja wa KMC Complex, Mwenge na kurudi kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Ahmed Ally mbele ya waandishi wa habari, amekanusha taarifa hizo kwa kusema. kuwa bado wapo sana na wataendelea kuwepo KMC Complex na ikitokea Simba inahama kwenye uwanja huo basi inakwenda kwenye uwanja wao wenyewe na si kwenda kwenye uwanja mwingine.