MAMA ONGEA NA MWANAO YA STEVE NYERERE YATOA BAISKELI ZAIDI YA 200.

Taasisi ya Mama ongea na mwanao imetoa zaidi ya baiskeli 200 pamoja na vyakula kwaajili ya watu wenye ulemavu (makundi maalum) kupitia kampeni ya “Asante Mama umetufikia” ikiwa na lengo la kulishika mkono kundi hilo.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama ongea na mwanao Steve Nyerere akiwa kwenye hafla hiyo Desemba 31 2024 amesema ni muhimu makundi maalum kufikiwa haswa kwenye shughuli za furaha kama za sikukuu ya mwisho wa mwaka ili nao wajisikie vizuri.

Katika salaam zake, Steve Nyerere amesema Rais Samia ameboresha mazingira kwaajili ya makundi hayo ikiwemo uboreshaji wa madarasa
katika vituo vyao wanavyoishi na kusomea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *