Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema kuwa Serikali imetangaza mchakato wa upanuzi wa barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Mto Mzinga ambayo itaenda mpaka Kongowe.
Ulega amesema Upanuzi huo wa barabara ya njia sita zenye, urefu wa kilomita 3.8, utakwenda sambamba na ujenzi wa daraja la kisasa la Mto Mzinga ili kurahisisha magari kupita kwa ufanisi katika eneo hilo linalokumbana na ajali.
Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), kwa sasa wapo katika michakato ya manunuzi itakayokamilika kati ya Januari na Februari 2025 kisha hatua ya kuwatafuta wakandarasi watakaotelekeleza mradi huo itafuata.