Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linaendelea kuwashikilia na kuwahoji watu wawili kwa uchunguzi juu ya tukio la kifo cha kutatanisha cha Mtoto wa mfanyabiashara maarufu Jijini Dodoma anayejulikana kwa jina la Jojo, Graison Kanyenye aliyekuwa na umri wa Miaka Sita, ambaye anadaiwa kuuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani wakati mama yake akiwa matembezini usiku wa kuamkia Disemba 25.
Akizungmza leo Disemba 27,2024 kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, George Katabazi amewataja watu hao kuwa ni mama Mzazi wa Marehemu (Jojo) na Kelvin Gilbert ambaye ni bodaboda aliyeachiwa mtoto.
“Hakuna kiwango cha mwisho kinachoonesha idadi ya watu lakini uchunguzi ndiyo utakao tuongoza ili haki iweze kutendeka,”amesema Kamanda wa Polisi.
Akijibu kuhusu kumshikiria Ofisa Uvuvi wa Mtera, Hamis Mohamed kama sehemu ya watuhumiwa wa tukio hilo ambaye walitoka na Jojo kwenda matembezini Kamanda Katabazi amesema baada ya uchunguzi kila kitu kitawekwa wazi hivyo kwasasa hawawezi kuingilia.
Pia ametumia wasaha huo kuwaomba wananchi wendelee kuwa watulivu wakati upelelei unaendelea kuhusu tukio hilo na kuendelea kuwakumbusha kutoa ushrikiano kwa jeshi la polisi kwa kuwaripoti waalifu.