‘SERIKALI INATAMBUA NA KUHESHIMU MCHANGO WA DINI ZA TANZANIA’ – MACHA.

NA EUNICE KANUMBA – SHINYANGA 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mh. Anamringi Macha amesema kuwa Serikali inatambua, inaheshimu na kuthamini kazi na mchango mkubwa unaotolewa na madhehebu ya dini likiwemo Kanisa Katoliki huku akiwaomba waumini kuendelea kumuombea baraka  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake ili aendelee kuwatumikia na kuwaletea maendeleo wananchi wake wakiwemo wa  mkoa wa Shinyanga.

RC Macha ameyasema hayo leo tarehe 19 Desemba 2024 katika ibada ya misa takatifu ya utoaji  wa daraja takatifu la Ushemasi kwa Deusdedith Nkandi  ilifanyika katika  kanisa kuu la mama mwenye huruma lilipo ngokolo jimbo katoliki la Shinyanga ambapo amempongeza shemasi kwa hatua hiyo huku akimuhaidi ushirikiano ili aweze kufikia malengo yake ya kuhubiri neno la Mungu.

RC Macha amesema  Serikali itaendelea kushirikiana na madhehebu ya dini katika kulinda Amani umoja na mashikamano huku akimtakia shemasi Nkani, utume mwema katika kuhubiri neno la Mungu na kutangaza upendo kwa msaada wa roho mtakatifu ambapo amemtaka pia  kwenda kuwahamasisha vijana wafanye kazi kwa bidii na waishi maisha mema yenye kumpende Mwenyezi Mungu

“Serikali inatambua, inaheshimu na inathamini sana mchango wa madhehebu ya dini zote likiwemo Kanisa Katoliki na kipekee kabisa nimpongeze Shemasi Nkandi na nimuahidi tu kuwa Serikali tutafanya naye kazi wakati wote na ukumbuke tu kuwa kwa kuwa wewe bado ni kijana, tunakutegemea sana kwenda kuwasaidia vijana wenzio waweze kuishi maisha mema ya kumpendeza Mungu na wafanye kazi pia kwa juhudi,” amesema RC Macha.

Ibada hii ya kumpandisha daraja Shemasi Nkandi  imeongozwa na Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akiwa na mwenyeji wake Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *