Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF), Patrice Motsepe anatarajia kuwasili nchini siku ya leo kwa ukaguzi wa viwanja vitakavyotumika katika mashindano ya CHAN pamoja na kuzungumza na kufanya vikao na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF.
Baada ya Kutoka Dar es salaam Disemba 20 Motsepe anatarajiwa kwenda Nairobi Kenya kukagua pia viwanja vitakavyotumika katika mashindano hayo pamoja na kikao na Shirikisho la mpira wa miguu nchini Kenya (FKF).
Kisha siku hiyo hiyo, Rais Motsepe ataunganisha safari yake kuelekea Kampala Uganda kufanya ukaguzi wa viwanja na Mkutano na uongozi wa Chama cha mpira wa miguu wa Uganda .
Mashindano ya CHAN yanatarajiwa kuanza rasmi kuanzia tarehe 1- hadi 28 ya mwezi Februari 2025.
Contact Us
P. O. BOX 71, Shinyanga, Tanzania
+255 766 408 253
info@jambofm.co.tz