ASKARI WAWILI WAFARIKI KWENYE MAPAMBANO NA MHALIFU DODOMA.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limetoa taarifa kwa umma kuwa tarehe 18.12.2024 majira ya saa saba usiku kwenye Kijiji cha Msagali Wilaya ya Mpwapwa Mkoa Wa Dodoma Askari Polisi D/Cpl. Jairo Boniface Kalanda na Pc. Alfred John walifariki dunia katika mapambano ya risasi wakati wakimkamata mtuhumiwa Atanasio Malenda,mwenye Miaka 30, Mkulima Mkazi wa kijiji cha Msagali.

Mtuhumiwa alikua anatuhumiwa kwa tuhuma za unyang’anyi wa kutumia silaha ambapo alilkuwa amemjeruhi Yohana Lameck na kumpora kiasi cha Tshs 2,000,000/= (Milioni mbili).

Hata hivyo Mtuhumiwa Atanasio Maleda nae amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu hospitali ya wilaya ya Mpwapwa kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa mapambano hayo.

Askari Polisi hao wakiwa na wenzao walipata taarifa kuwa mtuhumiwa huyo aliyekuwa

anatafutwa yuko nyumbani kwake katika Kijiji Cha Msagali na walifika Kijijini hapo na kutafuta Uongozi wa kijiji na kuelekea nao nyumbani kwa mtuhumiwa huyo, mara baada ya kufika mtuhumiwa huyo alitoka ndani na kuanza kuwashambulia askari na katika majibizano hayo ndipo vikatokea vifo hivyo.

Katika majibizano hayo askari D/pl. Msuka na raia mmoja anaefahamika kwa jina la Masima Nyau walijeruhiwa na wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *