‘MWAKA HUU HIFADHI YETU YA CHAKULA ITAFIKIA ZAIDI YA TANI LAKI SABA’ – WAZIRI BASHE. 

Waziri wa Kilimo Nchini Hussein Bashe ameomba radhi kwa ucheleweshwaji wa malipo ya nafaka kutoka Serikalini na kusema kuwa Serikali inafanyia kazi huku akitoa takwimu za malipo ambayo Serikali imeyafanya mpaka sasa.

Waziri Bashe kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ‘Salaam Ndugu Zangu, Nimekua nikipokea mirejesho kupita haya majukwaa ya kijamii na maswali mbali mbali juu ya malipo ya NFRA’. – Bashe.

‘Kwanza nikiri ni kweli kuna uchweleweshaji wa malipo na Serikali inafanyia kazi na tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliotokea, hadi kufikia hadi tarehe 11 Dec 2024 tumenunua nafaka zenye thamani ya Tsh 334.22 bilioni na tunadaiwa Tsh 52.4 bilioni ambazo zimebaki mikoa ya Songwe 6.8bn, 15.7 bn Rukwa na 29.8bn Ruvuma ambapo leo ljumaa tumeanza malipo ya kiasi cha Tsh 20.8bn ambapo tutalipa malipo kama ifuatavyo kwa Mfumo wa (FIFO)’ – Mh. Bashe.

Songwe 6.8bn

Rukwa 7bn

Ruvuma 7bn

‘Haya ni malipo tunayoya fanya leo na ni dhamira ya Serikali kuhakikisha kabla ya tarehe 10 Januari tuwe tumemaliza kulipa, Mwaka huu hifadhi yetu ya chakula itafikia zaidi ya tani 700,000 bila kuathiri utekelezaji wa mikataba ya Shirika la Chakula WFP na Serikali ya Zambia.’ – Mh. Bashe.

‘Ifahamike kuwa hii ni historia Serikali kununua NAFAKA kiwango hiki: ingawa zimetokea changamoto lakini naamini tutaendelea kurekebisha changamoto za mwaka huu ukiwemo mfumo wa malipo na mifumo yetu na Benki zetu za kibiashara ili kurahisisha malipo kwa wakati’. – Bashe

‘Tumedhamiria kuendelea kuboresha mfumo wetu wa malipo Na Msimu ujao utakao anza mwezi Juni/Julai tumejiwekea lengo la kununua tani 1.2m. Tunashukuru kwa ushirikiano. Kazi lendelee.’ – Mh. Bashe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *