Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Hali Ya ajira za Watoto Bado Ni Mbaya Nchini – Jaji Mstaafu Mwaimu

Na Gideon Gregory, Dodoma

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amesema hali ya ajira kwa Watoto bado ni mbaya jambo lililopelekea kuingizwa katika mpango kazi wa haki za binadamu na biashara.


Jaji Mwaimu ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akizungumza kwenye mkutano wa kitaifa wa wadau wa haki ya mtoto katika biashara huku akiongeza kuwa watoto bado wanatumikishwa katika sekta mbali mbali za kiuchumi


“Ndiyo maana tumeona wanastahili na wenyewe kuingizwa kwenye huu mpango kazi wa haki za binadamu na biashara na inafanyika hivyo kwasababu nadhani bado mnatambua kwamba watoto bado wanatumikishwa katika biashara hivyo eneo hili kufanyiwa kazi ni sehemu ya mkakati ambao utasaidia na baada ya mpango kazi huu kuandaliwa panaweza kuwa na masuala ya elimu kwa wafanyabiashara ili waweze kuona umuhimu wa kuto ajiri watoto,”amesema.


Ameongeza kuwa mtoto kufanya kazi ni haki yake ya msingi lakini sio zile kazi ambazo zinawaumiza watoto na kuwaacha na majeraha.


Awali akifungua mkutano huo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Flanklin Rwezimula amewaomba washiriki katika mdahalo huo kuweka mipango na mikakati maalum ya kumlinda mtoto.


Sanjari na hayo ameihakikishia THBUB kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao ili iweze kutimiza majukumu yake kikamilifu.


Nae Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Ndogondogo Mkoa wa Dodoma kupitia Shirikisho la Umoja wa Wamachinga Tanzania (SHIUMA), Christian Msumari amekiri kuwa changamoto hiyo ipo katika maeneo yao na watoto wanakumbana na mazingira magumu.


“Mimi kama kiongozi ambaye nipo kwenye nyaja ya biashara na wafanyabiashara ndogondogo hiyo naomba nikiri kweli hiyo changamoto ipo katika maeneo yetu ya masoko na maeneo yetunya biashara kwasababu kwenye haya ni maeneo watu wengi wenye kipato kidogo wanaingia kwasababu ni sehemu ambayo inaruhusu watu wote kuingia “amesema.

Amesema kuwa watoto wadogo wanaingia kwenye ajira na mazingira wanayokutana nayo sio rafiki kulingana na umri walionao na waliyolelewa na hivyo wanachukua tabia tofauti na kujikuta wanaingia kwenye mfumo wa malezi ambao sio rasmi.


Mratibu wa Chama Cha wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA), Neema Ahmed amesema wao kama wadau wanatoa msaada wa kisheria na kuchangia katika mpango huo ili kuona ni namna gani utaboresha upatikanaji wa haki za watoto hususani wale walioingizwa kwenye ajira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *