Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mahakama Nchini Uganda Yawatia Hatiani Wanachama 16 Wa Upinzani Kwa kosa la Uhaini

Chanzo: Dw

Mahakama ya kijeshi nchini Uganda imewatia hatiani wanachama 16 wa chama cha upinzani kwa kosa la uhaini na umiliki wa vilipuzi kinyume cha sheria.


Taarifa hiyo ni kulingana na wakili wa upande wa utetezi Shamim Malende, ambaye amesema kesi hiyo ilikuwa na mashaka kutokana na jinsi ilivyosikilizwa na baadaye watuhumiwa kukubali makosa ambayo awali waliyakana.


Upande wa mashtaka umedai kuwa wanachama 16 wa Jukwaa la Umoja wa Kitaifa (NUP), pamoja na wengine ambao bado hawajakamatwa, walikutwa na vilipuzi kati ya Novemba mwaka 2020 na Mei 2021, wakati ambao uchaguzi ulikuwa ukiendelea.
Vijana hao 16 wamekaa gerezani kwa miaka minne, na watafikishwa mahakamani Octoba 23, 2024 ili kusomewa rasmi hukumu yao.


Kwa upande wake Mwimbaji wa zamani na kiongozi wa upinzani Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine , amedai kuwa watu hao walilazimishwa kukiri makosa yao na kuomba msamaha wa rais.


“Chochote ambacho serikali ya Museveni inafanya, siku moja wale wote walio chini yake akiwemo yeye mwenyewe watawajibishwa” alisema Bobi Wine, akisisitiza kuwa washtakiwa “walilazimishwa na maafisa wa serikali kukubali makosa hayo”.


Tangu mwaka 1986, Uganda imetawaliwa na rais Yoweri Museveni na katika uchaguzi uliopita wa urais wa mwaka 2021 ulikumbwa na kashfa ya udanganyifu, na maandamano ya kupinga kukamatwa tena kwa Bobi Wine yalikandamizwa vikali na polisi, na kusababisha takriban watu 54 kuuawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *