Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mkuu Wa Chuo cha IAA Afikishwa Mbele Ya Baraza La Maadili

Na Gideon Gregory


Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma imemfikisha mbele ya Baraza la maadili, Mkuu wa Chuo cha Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamin Sedoyeka kwa malalamiko Manne ya kukiuka maadili ya viongozi wa umma.


Akisoma malalamiko yanayomkabili Prof. Sedoyeka leo Jijini Dodoma mbele ya Mwenyekiti Jaji Mstaafu Rose Teemba Wakili wa Serikali Emma Gelani amesema malalamiko hayo yaliwasilishwa Septemba 15,2024 ambayo ni pamoja na Kumpandisha cheo bila kufuata taratibu za utumishi wa umma Bw. Hakimu Ndatama kutoka afisa Rasilimali daraja la Pili kuwa mkuu wa sehemu ya rasilimali watu kabla ya kukamilika kwa uhamisho wa mtumishi huyo na bila kuwa na sifa.


Lingune ni Kufanya uhamisho wa ndani wa mtumishi Bw. Robert Mwitango kutoka kitengo cha ununuzi na ugavi kwenda Idara ya Maktaba tofauti na sifa za kitaaluma za mtumishi huyo kuwa ni ununuzi na ugavi bila kuzingatia sheria, Kuingilia mchakato wa zabuni ya ununuzi na ufugaji wa viti na meza katika Kampasi ya chuo hicho Babati kwa kuifuta bila kufuata utaratibu na bila sababu za kisheri pamoja na mgongano wa kimaslahi.


Akitoa ushahidi mbele ya Baraza hilo Afisa wa Sekretarieti ya maadili kwa viongozi wa Umma Dodoma Ramadhan Mwanang’waka amesema katika uchunguzi wao walibaini kuwa mlalamikiwa alifanya uteuzi wa mtumishi Hakimu Ndatama kuwa mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu kinyume na sheria na taratibu kwasababu mtumishi huyo aliteuliwa katika wadhifa huo wakati alikuwa mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na alikuwa akifanya kazi kwa kuazimwa katika chuo hicho.


Shahudi huyo amesema kingine walichokibaini ni kuwepo kwa mgongano wa mslahi kwa Mkuu huyo katika majukumu yake ikiwemo suala la upendeleo kwa mtumishi huyo kwa kumteua katika nafasi ya uongozi hali kuwa ni mtumishi ambaye alikuwa ni Afisa daraja II na hakuwa nasifa za kuteuliwa kuwa mkuu wa Taasisi katika utumishi wa umma.


Mlalamikiwa alijitetea kufanya teuzi hizo kwa kusema kuwa alikuwa akimuamini, licha ya kuwa wakati anateuliwa mtu huyo kwenye kitengo hicho alikuwepo afisa mwingine ambaye alikuwa na sifa za kuteuliwa kuwa mkuu wa idara tofauti na yule aliyeteuliwa ambaye Prof. Sedoyeka anadai alimsomesha mtu huyo mpaka kumuamini na kumpatia cheo ila baada ya kuulizwa kwanini kafanya hivyo alisema hakuwa na umahili wa nafasi hiyo.


Shauri hilo lenye jumla ya mashahidi wane linaendelea leo octoba 17 2024.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *