Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mashabiki wa Wizkid na Burna Boy wasikitishwa na taarifa za Forbes kumtaja Davido kama msanii tajiri zaidi Afrika 2024.

Mashabiki wa nyota wa muziki wa Nigeria ‘Wizkid’ na ‘Burna Boy’ wamesikitishwa na Taarifa ya Jarida la Biashara la Marekani la Forbes, baada ya kumtaja mwanamuziki ‘Davido’ kama msanii tajiri zaidi barani Afrika kwa 2024.

Orodha hiyo ambayo imesubiriwa kwa hamu na mashabiki imeorodhesha wasanii watano bora wa Kiafrika, akiwemo ‘Wizkid’, ‘Burna Boy’, ‘Rema’, na ‘Don Jazzy’. Davido akitwaa taji la msanii tajiri zaidi barani Afrika akiwa na utajiri wa dola milioni 100 ( Bilioni 272Tsh).

Akifuatiwa na ‘Don Jazzy’ dola milioni 50 (Bilioni 136 Tsh), Burna Boy dola milioni 30 (Bilioni 81.6Tsh), ‘Wizkid’ dola milioni 25 (Bilioni 68Tsh), na ‘Rema’ dola milioni 15 (Bilioni 40.8Tsh).

Akifuatiwa na ‘Don Jazzy’ dola milioni 50 (Bilioni 136 Tsh), Burna Boy dola milioni 30 (Bilioni 81.6Tsh), ‘Wizkid’ dola milioni 25 (Bilioni 68Tsh), na ‘Rema’ dola milioni 15 (Bilioni 40.8Tsh).

Taarifa hiyo imezua mijadala katika mitandao ya kijamii. Ikumbukwe kuwa mwanamuziki ‘Rema’, katika moja ya nyimbo zake, ametaja kwamba enzi ya “Big Three” imekwisha kwa sababu sasa anakuwa wa nne nakuitangaza “Big Four”, jambo ambalo lilichochea mjadala zaidi kati ya mashabiki.

Orodha hii imezusha kutoelewana kati ya wapenzi wa muziki, haswa mashabiki wa ‘Wizkid’ na ‘Burna Boy’, ambao hawakufurahishwa na matokeo.

Hii inakuja huku kukiwa na ugomvi unaoendelea mtandaoni kati ya ‘Davido’ na ‘Wizkid’, ambao umezidi kuibua hisia ndani ya mashabiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *