Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Tarura mkoa wa Geita imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni 1 kuboresha mawasiliano ya miundombinu ya barabara

Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mjini (Tarura) Mkoa wa Geita imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni 1.7 kwa lengo la kurejesha mawasiliano ya barabara zote zilizoharibiwa na mvua katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Tarura Mkoa wa Geita Mhandisi David Msechu wakati akizungumza na Jambo Fm ambapo amesema kutokana na mvua hizo zilizonyesha kuanzia mwaka wa fedha 2023/24 zilipelekea uharibifu mkubwa wa barabara na sasa tayari serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 1.7 kwa ajili ya ukarabati wa barabara zilizoharibiwa na mvua hizo.

Aidha amesema kutokana na uharibifu huo uliopelekea pia kukatika kwa mawasiliano ya daraja linalounganisha Wilaya ya Geita na Nyang’hwale tayari Milioni 500.3 zimeshatolewa kwaajili ya kuanza ujenzi wa daraja hilo ili kurejesha mawasiliono kati ya wilaya hizo ambazo ni muhimili muhimu wa utoaji huduma mbalimbali kwa wananchi.

Uharibifu huo wa barabara uliosababishawa na mvua kubwa za msimu uliopita ulipelekea asilimia 47 ya barabara zinazohudumiwa na Tarura Mkoa wa Geita kutopitika kabisa hivyo kutokana na jitihada mbalimbali zilizofanywa na serikali ikiwemo ukarabati wa baadhi ya miundombinu kwa sasa zaidi ya asilimia 70 barabara hizo zinapitika na kwa ujumla ukarabati huo unatarajiwa kukamilika Novemba Mwaka huu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *