Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mama mzazi azua taharuki kwa madai ya mtoto wake kupigwa na mwalimu mpaka kufa – Mwanza

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linamshikilia Christina Joshua (35) mkazi wa Bugarika kwa kosa la kuzua taharuki kuwa mtoto wake amepigwa na mwalimu hadi kusababisha kifo chake.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema mtuhumiwa huyo ambae ni mama mzazi wa Leonia Amir (16) mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Mlimani alisambaza taarifa kuwa mwanae ameuawa kwa kupigwa na mwalimu hadi kusababisha umauti hali iliyofanya wananchi wakusanyike katika shule hiyo kwa lengo la kufanya vurugu.

Mara baada ya kupokea taarifa hizo Jeshi la polisi lilifika katika shule hiyo na kukuta wananchi wakiwa na hasira kali huku mama wa mtoto huyo akiwa analia.

Katika mahojiano ya awali mama huyo amesema alipokea taarifa kutoka kwa watu kuwa mtoto wake anaesoma katika shule ya sekondari Mlimani amepigwa na mwalimu wake na kupoteza maisha.

Aidha Mutafunga amesema kufuatia uwepo wa taharuki hiyo Jeshi la polisi lilimtafuta mtoto huyo na kumkuta hai na walipo mhoji alisema kuwa hakupigwa wala kugombezwa na mwalimu yoyote na tayari Jeshi hilo linamshikilia Mama wa mtoto huyo kwa ajili ya maho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *